Home Habari Kuu Waziri Machogu alalama ongezeko la uvamizi shuleni

Waziri Machogu alalama ongezeko la uvamizi shuleni

0
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amelalamikia ongezeko la visa vya uvamizi wa shule kutokana na matokeo duni katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE.

Machogu kwenye taarifa kwa vyombo vya habari amesema pia baadhi ya walimu wameshambuliwa tangu atangaze matokeo Januari 8.

Waziri amesisitiza kuwa matokeo ya wanafunzi katika mitihani ya kitaifa yanatokana na mchango wa wadau wote na sio walimu pekee.

Badala yake waziri amewataka wote wasioridhishwa na matokeo kuwasilisha kesi mahakamani.

Website | + posts