Home Habari Kuu Waziri Linturi afanya mabadiliko katika usimamizi wa mashirika kadhaa

Waziri Linturi afanya mabadiliko katika usimamizi wa mashirika kadhaa

0

Waziri wa kilimo Mithika Linturi ametangaza mabadiliko katika usimamizi wa mashirika manne ya serikali katika juhudi za kuyalainisha na azimio la serikali ya Kenya Kwanza la kuhakikisha uwepo wa chakula cha kutosha wakati wote humu nchini.

Linturi ametetea mabadiliko hayo akisema ni ya manufaa kwa nchi hii.

Kwenye mabadiliko hayo, Daktari Seth Ooko Onyango ameteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa baraza la kukabiliana na mbung’o na ugojwa wa malale – KENTTEC.

Frederick Njiru Muchiri Sasa ndiye mkurugenzi mtendaji wa bodi inayodhibiti bidhaa za kukabiliana na wadudu waharibifu – PCPB, huku Bernadette Jeptoo Misoi akiteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa kituo cha raslimali za aina bora ya mifugo KAGRIC.

Kampuni ya sukari ya Chemelil nayo ina mkurugenzi mtendaji mpya kwa jina Moses Kiprop Kolum.

Waziri huyo wa kilimo amekuwa akitekeleza mabadiliko kama hayo kwa muda sasa huku mengine yakitarajiwa mwakani.

Website | + posts