Home Kimataifa Waziri Kindiki kwenye ziara ya siku tatu, Lamu

Waziri Kindiki kwenye ziara ya siku tatu, Lamu

0
Waziri wa Usalama wa Taifa Kithure Kindiki aanza ziara ya siku katika kaunti ya Lamu
Waziri wa Usalama wa Taifa Kithure Kindiki aanza ziara ya siku katika kaunti ya Lamu
kra

Waziri wa Usalama wa Taifa Prof. Kithure Kindiki leo Alhamisi ameanza ziara ya siku tatu katika kaunti ya Lamu.

Wakati wa ziara hiyo, Prof. Kindiki anasema atafanya msururu wa mikutano na Kamati ya Usalama na Ujasusi ya Kaunti hiyo na viongozi wa kisiasa, kidini, biashara na jamii pamoja na raia wa eneo hilo.

kra

Punde alipowasili, alifanya mkutano na Kamati za Usalama na Ujasusi za Kaunti ya Lamu na Kaunti Ndogo ya Lamu Magharibi katika eneo la Witu.

Kaunti ya Lamu imekumbwa na visa vya ukosefu wa usalama siku zilizopita ambavyo vilisababisha vifo vya watu kadhaa na mali kuharibiwa.

Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab linasalia kuwa tishio kwa eneo hilo.

Waziri Kindiki anasema ugaidi na uhalifu wa kuvuka mpakani unaongoza kwenye orodha ya matishio dhidi ya usalama wa kitaifa na kuongeza kuwa serikali itaendelea kuwapa vifaa maafisa wa usalama kutoka vitengo mbalimbali ili kukabiliana na uhalifu wa kisasa na kuzuia uvamizi unaonfanywa na makundi ya kigaidi.

Website | + posts