Home Taifa Waziri Kindiki aelezea masharti ya kuzingatiwa wakati wa maandamano

Waziri Kindiki aelezea masharti ya kuzingatiwa wakati wa maandamano

0
kra

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof. Kithure Kindiki ameelezea masharti kadhaa yanayopaswa kuzingatiwa na waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024. 

Waandamanaji hasa vijana wanaofahamika kama Gen Z wamepanga kufanya maandamano makubwa kesho Jumanne kupinga mswada huo.

kra

Miongoni mwa mambo mengine, amewataka waandamanaji kuhakikisha wanazingatia sheria wakati wote.

Amesema maandamano hayo yanapaswa kumalizika kufikia saa 12:30 jioni bila kusababisha hata chembe moja ya usumbufu.

“Lazima wasitishe shughuli zao machweo au saa 12:30 jioni, yoyote itakayotangulia, kwa mujibu wa Sheria ya Utaratibu wa Umma Kipengele cha 57 cha sheria za Kenya,” alisema Kindiki wakati akiwahutubia wanahabari leo Jumatatu.

“Ni sharti wasifanye uchokozi, kumshambulia au kuzuia maafisa wa usalama au hata umma. Hawapaswi kuzuia, kuziba au kuharibu mali yoyote binafsi  au ya umma. Ni lazima wazingatie sheria za nchi ya Kenya ikiwa ni pamoja na sheria ya ulinzi wa maeneo ambayo inazuia ufikiaji wa miundombinu fulani muhimu kwa ajili ya sababu za usalama.”

Kadhalika, Waziri Kindiki amewataka waandamaji kuelezea barabara watakazotumia wakati wa maandamano hayo ili maafisa wa usalama wahakikishe wanapatiwa ulinzi wa kutosha.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here