Home Habari Kuu Waziri Kindiki abuni maeneo mapya ya utawala katika kaunti 31

Waziri Kindiki abuni maeneo mapya ya utawala katika kaunti 31

0

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof. Kithure Kindiki amebuni maeneo mapya ya utawala katika kaunti 31 kwa kusudi la kuboresha uratibu wa huduma za serikali nchini.

Kupitia gazeti rasmi la serikali lililochapishwa Februari 14, 2024, Waziri Kindiki amebuni kaunti ndogo 16 ambazo ni Tarasaa, Tiriki East, Narok Amalo, Kambu, Murera, Kerio Valley, Kabras East, Kabras West na Usigu.

Kaunti zingine ndogo zilizobuniwa ni Suba Central, Suba West, Suba South, Rachuonyo West, Dagoretti North na Dagoretti South.

Kaunti za Kilifi, Lamu, Wajir, Mandera, Tharaka Nithi, Embu, Makueni na Kakamega ni miongoni mwa kaunti ambazo maeneo mapya ya utawala yamebuniwa ikiwa ni pamoja na divisheni, kata na kata ndogo.

Ili kupata taswira kamili ya maeneo mapya ya utawala yaliyobuniwa, unaweza ukataza gazeti rasmi la serkali lililochapishwa jana Jumatano kwa kutembelea linki ifuatayo:

https://www.interior.go.ke/wp-content/uploads/2024/02/gazette-vol.-17-14-2-24-special-admin-units.pdf

 

 

Website | + posts