Home Taifa Waziri Kindiki abuni kamati ya kitaifa ya kuongoza utekelezaji wa mabadiliko katika...

Waziri Kindiki abuni kamati ya kitaifa ya kuongoza utekelezaji wa mabadiliko katika vikosi vya usalama

0
kra

Waziri wa usalama wa taifa Kithure Kindiki ameteua kamati ya kitaifa ya kuongoza utekelezaji wa mabadiliko yaliyopendekezwa na jopo lililokuwa likiongozwa na jaji mkuu mstaafu David Maraga katika vikosi mbali mbali vya usalama nchini.

Vikosi hivyo ni pamoja na huduma ya kitaifa ya polisi, huduma ya magereza nchini na huduma ya vijana kwa taifa NYS.

kra

Mwenyekiti wa kamati hiyo ni katibu wa usalama wa ndani Raymond Omollo na makatibu wa idara za fedha, huduma za urekebishaji, utumishi wa umma na masuala ya baraza la mawaziri watakuwa wanachama.

Wanachama wengine wa kamati hiyo ni pamoja na wakili wa serikali, inspekta jenerali wa polisi, Kamishna jenerali wa huduma ya magereza, kamishna jenerali wa huduma ya vijana kwa taifa na mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya huduma ya vijana pamoja na mwenyekiti wa mamlaka huru ya kutathmini utendakazi wa polisi.

Afisi ya mkuu wa utumishi wa umme,afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma, tume ya utumishi wa umma, tume ya mishahara na marupurupu, baraza la kitaifa la huduma ya vijana kwa taifa na tume ya kurekebisha sheria ya Kenya pia zitawakilishwa kwenye kamati hiyo.

Kamati hiyo iliyotangazwa kwenye arifa ya gazeti rasmi la serikali tarehe 13 mwezi Septemba mwaka 2024, itahudumu kwa muda wa miaka mitatu.

Jopo la kitaifa la mabadiliko katika vikosi vya usalama lilipendekeza mabadiliko kadhaa katika vikosi vya usalama kama vile kuongezwa kwa mishahara, mazingira bora ya kikazi, makazi ya hadhi kwa polisi kati ya mapendekezo mengine mengi.

Tayari serikali imetangaza nyongeza ya mishahara ya maafisa wa polisi.

Website | + posts