Home Kimataifa Waziri Chirchir na Siror waagizwa kufika bungeni

Waziri Chirchir na Siror waagizwa kufika bungeni

0
Davis Chirchir na Joseph Siror
kra

Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu kawi imemwagiza waziri wa kawi Davis Chirchir na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya umeme nchini Kenya Power Joseph Siror kufika mbele yake Alhamisi wiki ijayo kuelezea kuhusu ukosefu wa umeme uliokumba nchi nzima Ijumaa hadi Jumamosi.

Chini ya uenyekiti wa mbunge wa eneo la Mwala Vincent Musyoka, kamati hiyo ya bunge ya kawi inataka wawili hao kuelezea kwa kina kuhusu kilichosababisha umeme kupotea nchini na kuathiri sehemu kadhaa muhimu kama vile uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA.

kra

Haya yanajiri wakati ambapo kampuni ya Kenya Power imetoa taarifa kwa umma kuelezea kwamba ililazimika kuhuisha kiunganishi cha umeme cha Uganda ili kuweza kurejesha huduma zake za umeme nchini.

Taarifa hiyo ilielezea kwamba ililazimika pia kutumia nguvu za umeme kutoka kituo cha umeme cha Seven Fork kuanzisha mashine zake ilipokuwa ikisubiri kiunganishi kutoka Uganda.

Kulingana na KPLC, nguvu za umeme kutoka bwawa la Seven Fork huchukua muda ikilinganishwa na umeme kutoka Uganda.

Kutokana na kupotea kwa umeme katika uwanja wa ndege wa JKIA Ijumaa usiku, waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen alimtimua mkurugenzi mtendaji wa mamlaka inayosimamia viwanja vya ndege humu nchini Alex Gitari.