Home Habari Kuu Waziri Namwamba ashauriana na mwakilishi wa UNDP kuhusu masuala ya viajana

Waziri Namwamba ashauriana na mwakilishi wa UNDP kuhusu masuala ya viajana

0

Waziri wa Mambo ya Vijana, Sanaa na Michezo Ababu Namwamba alishiriki mazungumzo na mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo, UNDP Ahunna Eziakonwa, ambaye ni msimamizi msaidizi na mkurugenzi mkuu wa afisi ya bara Afrika ya shirika hilo kuhusu ushirikiano katika masuala ya vijana na ubunifu.

Waziri Namwamba alisema wizara yake imejitolea kuwezesha, kuhamasisha na kukuza ajenda ya ubunifu kati ya vijana kuambatana na mpango wa serikali wa kuwainua kiuchumi watu wa tabaka la chini almaarufu “Bottom-Up Economic Transformation Agenda – BETA”.

Waziri alisema vijana ni rasilimali ambayo lazima wawekeze kwayo ili wapate mazuri katika kuendeleza nchi zao.

“Hebu tuanzishe utamaduni wa kujumuisha wote, ambapo tutahamasisha na kujuisha vijana wetu katika maamuzi muhimu ya mataifa ili tuunde mazingira ambapo idadi kubwa ya rasilimali watu inahusishwa katika uundaji sera za vijana kwa ajili ya vijana” alisema waziri.

Waziri alipongeza Kenya kwa kuteuliwa kati ya mataifa manane amayo yanahusika pakubwa katika kuanzisha kituo cha kuwapa wabunifu nafasi ya kutekeleza uchunguzi wao na kuhifadhi msisimko wa Afrika.

Alisema ubunifu ndio nguzo kuu ya siku zijazo na ujuzi ndio hujenga maendeleo na kuwezesha watu kutumia fursa zilizopo.

Talanta pia alisema ni muhimu katika kusuluhisha tatizo la ukosefu wa ajira kati ya vijana, ndiposa wakaanzisha mpango wa Talanta Hela ili kusaidia vijana kugeuza talanta zao kuwa ajira.

Bi. Ahunna Eziakonwa kwa upande wake alisema ipo haja ya majadiliano, uwezeshaji na uundaji wa fursa kwa vijana katika njia ambazo zitawafanya wawe sehemu ya mazungumzo yanayoendelea.

Alimsifia waziri Nambwamba na serikali ya Kenya kwa kuanzisha mpango wa #TalantaHela ambao unaunganisha michezo na ubunifu na kuzigeuza kuwa njia za kujipatia mapato ili kuinua maisha.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here