Home Michezo Waziri Ababu akagua ukarabati uwanjani Kasarani

Waziri Ababu akagua ukarabati uwanjani Kasarani

0

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba, alifanya ukaguzi wa ghafla wa ukarabati unaoendelea katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kwa maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2027.

Waziri alifanya ziara hiyo Jumatano jioni akiandamana na Mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya viwanja nchini Piua Metti.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba akifanya ukaguzi wa ukarabati unaofanywa uwanjani Kasarani

Waziri alitoa hakikisho la serikali kukamilisha ukarabati huo kwa wakati unaofaa, ili kuwa tayari kwa ukaguzi utakaofanywa na shirikisho la kandanda barani Afrika CAF mwaka 2025.

Waziri Ababu Namwamba akikagua ukarabati uwanjani Kasarani

Ababu aliipongeza wizara ya ulinzi inayoendesha ukarabati huo, wakilenga kuafiki viwango vya kimataifa vinavyohitajika na CAF na FIFA.

Kasarani,Nyayo na Kipchoge Keino sawia na uwanja mwingine mpya wa Talanta utakaojengwa eneo la Jamhuri, vimeratibiwa kuandaa kipute cha AFCON mwaka 2027.

Kenya itaandaa kindumbwendumbwe hicho kwa pamoja na Tanzania na Uganda.