Home Michezo Waziri Ababu akagua ujenzi wa uwanja wa Afraha

Waziri Ababu akagua ujenzi wa uwanja wa Afraha

0

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba  siku ya Ijumaa amekagua ukarabati wa uwanja wa Afraha Nakuru na kubaini uwezo wa uga huo kuandaa mashindano ya michezo.

Ababu amesema kuwa serikali ya kitaifa itashirikiana na serikali ya kaunti ya Nakuru kuhakikisha uwanja wa Afraha unaafiki viwango vya kimatifa vya FIFA na CAF.

Kulingana na Waziri Ababu uwanja wa Afraha utapanuliwa kumudu idadi ya mashabiki 15,000.