Home Michezo Waziri Ababu afungua rasmi uwanja wa Kiprugut Chumo

Waziri Ababu afungua rasmi uwanja wa Kiprugut Chumo

0

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amezindua rasmi uwanja wa Kiprugut Chumo katika kaunti ya Kericho.

Waziri amefungua uwanja huo Jumamosi takriban mwezi mmoja baada ya uwanja huo uliojulikana kama Kericho Green kuandaa sherehe za Mashujaa kufuatia kufanyiwa ukarabati.

Ababu aliandamana na katibu wake Mhandisi Peter Tum, Rais wa chama cha Riadha Kenya Jackson Tuwei, na Mkurugenzi wa halmashauri ya viwanja nchini Pius Metto .

Uga huo ulipewa jina la Kiprugut Chumo kwa heshima ya Mkenya wa kwanza kunyakua medali katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 1964 marehemu Wilson Kiprugut, na Rais William Ruto wakati wa sherehe za Mashujaa.

Marehemu Chumo alikuwa mzaliwa wa kaunti ya Kericho.

Website | + posts