Home Kimataifa Wazee wa vijiji kupokea marupurupu

Wazee wa vijiji kupokea marupurupu

0
kra

Kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa imeidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 4 kila mwaka ambazo zitatumika kuwapa wazee wa vijiji marupurupu ya kila mwezi.

Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ilikubalia kuchapishwa kwa mswada wa uratibu katika serikali kuu na iwapo utapitishwa, kila mzee wa kijiji atakuwa akipokea shilingi elfu 7 kila mwezi.

kra

Mswada wa uratibu wa serikali kuu umedhaminiwa na mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse na unatafuta kuilazimisha serikali kuwalipa wazee wa vijiji kutokana na jukumu lao muhimu la kuratibu ajenda ya serikali mashinani.

Wazee hao watapokea marupurupu ya shilingi elfu 4 kila mmoja kwa mikutano minne itakayoandaliwa na chifu, marupurupu ya shilingi 2,000 ya usafiri kila mwezi na marupurupu ya masalio ya simu ya shilingi elfu moja kila mwezi.

Mbunge wa Kibwezi Magharibi ana imani kwamba marupurupu hayo yatasaidia kuboresha uratibu wa mipango ya serikali.

Kamati ya bunge kuhusu bajeti iliunga mkono pia kutolewa kwa shilingi milioni 258 kila mwaka ambazo zitasaidia kutoa uhamasisho kwa umma kuhusu makosa ya ubakaji.

Website | + posts