Home Kimataifa Wazazi wahimizwa kutowaficha watoto walemavu

Wazazi wahimizwa kutowaficha watoto walemavu

Alisema watoto hao hunyimwa haki ya kupata elimu, kuonyesha talanta na ujuzi wanapofungiwa nyumbani.

0
Mchungaji Dorcas Rigathi.
kra

Mke wa naibu Rais, mchungaji Dorcas Rigathi, ametoa wito kwa wazazi kutowaficha watoto walio na ulemavu, badala yake wahakikishe wanapata elimu.

Akizungumza katika shule ya Kizurini, kaunti ndogo ya Kaloleni, kaunti ya Kilifi, Dorcas aliwahimiza wazazi kuwaonyesha upendo watoto walemavu, badala ya kuwaficha.

kra

Alisema watoto hao hunyimwa haki ya kupata elimu, kuonyesha talanta na ujuzi wanapofungiwa nyumbani.

“Mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Nawashukru wazazi waliowaleta watoto wao shuleni. Watoto ni watu wa ajabu sana,’ alisema Dorcas.

Mchungaji huyo aliwaeleza wale wanaoishi na ulemavu kwamba hakuna kitakachowazuia kuafikia ndoto zao maishani.

“Unapowaona hawa watoto, waonyeshe upendo, wapeleke shuleni. wengi wao ni werevu. Na nyinyi watoto hakuna kizuizi, nyinyi ni bora zaidi na ninafurahia kuwa mama yenu,” aliongeza Mchungaji Dorcas.

Alitoa msaada wa chakula, viti vya magurudumu pamoja na vitu vingine vya kimsingi.