Home Kaunti Wavulana waliofariki baada ya kubugia Ethanol wazikwa leo

Wavulana waliofariki baada ya kubugia Ethanol wazikwa leo

0

Miili ya watahiniwa wawili wa mtihani wa kidato cha nne KCSE ambao walifariki baada ya kubugia Ethanol wiki jana imezikwa leo.

Wavulana hao wawili walikuwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya mseto ya Karigini katika wadi ya Muthambi, kaunti ya Tharaka Nithi.

Jumla ya wanafunzi 13 walihusika kwenye kisa hicho cha kunywa kile kinachoaminika kuwa Ethanol shuleni humo.

Wawili kati yao waliaga dunia, huku wengine wavulana wanane na wasichana watatu wakikimbizwa kwenye hospitali iliyo karibu na shule hiyo.