Home Kaunti Waumini washerehekea miaka 100 ya kanisa la St. Johns ACK Kaloleni

Waumini washerehekea miaka 100 ya kanisa la St. Johns ACK Kaloleni

0
kra

Kulikuwa na shangwe na nderemo katika eneo la Kaloleni Giriama wakati mamia ya waumini walikuwa wakisherehekea miaka 100 tangu kanisa la St Johns ACK lilipojengwa na wamishonari.

Jengo la kanisa hilo lililojengwa na wamishonari hao bado limesimama kwa muundo huo huo hadi leo.

kra

Sherehe hizo ambazo pia zilijumuisha maadhimisho ya miaka 120 tangu injili ya Yesu ilipofikishwa katika eneo hilo, ziliongozwa na Askofu wa dayosisi ya Mombasa Alphonce Baya Mwaro Pamoja na Askofu mstaafu Julius Kalu.

Miongoni ya waliohudhuria ni Mama Sarah Mwachisenge wa umri wa miaka 121 ambaye ndiye muumini wa pekee aliyesalia kati ya walioanzisha dini na wamishonari katika kanisa hilo.

Wengine ni Pamoja na Naibu Gavana wa Kilifi flora Chibule, aliyekuwa Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana na aliyekuwa mkuu wa majeshi Jenerali Samson Mwathethe.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Pwani na kile cha Technical cha Mombasa ambao walinakili historia ya kanisa na dini pia walihudhuria ibada hiyo ya maadhimisho.

Kando na kujenga kanisa hilo ambalo ni muhimu kihistoria, wamishonari walijenga pia shule ya upili ya wasichana ya Mtakatifu Yohana inayojulikana sana nchini na hospitali ya Mtakatifu Luka.

Waliwezesha wakazi kupata injili, huduma za matibabu na elimu.

Kumbu kumbu za wamishonari zilikuwa wazi na askofu akawahimiza wafuasi kuendeleza injili ya Kristo.

Website | + posts
Dickson Wekesa
+ posts