Wauguzi wanaotaka kufanya kazi ughaibuni sasa hawatahitaji kusafiri nje ya nchi ili kwenda kufanya mitihani ya kuwakubalia kufanya kazi katika nchi mbalimbali duniani.
Hii ni baada ya kituo cha mitihani ya wauguzi wanaotaka kufanya kazi ughaibuni kuanzishwa hapa nchini Jana Jumanne.
Kituo hicho kinajulikana kama “The Pearson Virtual Universal Enterprises, (VUE).
Awali, wauguzi walitakiwa kusafiri hadi nchini Afrika Kusini ili kufanya mitihani ya kuwakubalia kufanya kazi katika hizo.
“Hata wale wanaotaka kwenda Marekani, zamani ulikuwa uende mpaka South Africa, huko ndio kulikuwa na examination centre. Sasa Wamarekani wamekubali tuwe na examination centre Kenya na ilianzishwa jana,” alisema Rais Ruto wakati akiwahutubia wakazi wa eneo bunge la Endebess leo Jumatano.
“Tutakuwa tunafanya examination yetua ya kupeleka nurses kule duniani hapa Kenya.”
Rais Ruto akiashiria kuwa kundi la kwanza la wauguzi 2,500 liko mbioni kuelekea nchini Saudia ambayo imetoa jumla ya nafasi nusu milioni kwa wauguzi kutoka Kenya kuhudumu nchini humo.
Ruto aliwataka wauguzi kuwa mstari wa mbele kutuma maombi akiwahakikishia kuwa mapato yatakuwa mazuri.