Home Habari Kuu Watu zaidi ya laki 8 watoroka Rafah

Watu zaidi ya laki 8 watoroka Rafah

0
kra

Philippe Lazzarini mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia wakimbizi wa Palestina UNRWA amesema kwamba watu zaidi ya elfu 800 wametoroka mji wa Rafah tangu Israel ilipoanza kutekeleza mashambulizi kwenye mji huo wiki iliyopita.

Kupitia taarifa aliyotoa jana Jumamosi, Lazzarini alilalamikia kile alichokitaja kuwa kufurushwa mara kwa mara kwa wa Palestina tangu vita kati ya Israel na Hamas vilipoanza Oktoba mwaka jana.

kra

Alisema watu hao wamekuwa wakifurushwa hata kutoka kwenye kambi za UNRWA.

Mkuu huyo wa UNRWA anasema watu wanapohama usalama wao unahatarishwa kwani hawana mapito salama au ulinzi unaofaa na wanalazimika kuacha baadhi ya mali zao ambazo hawana uwezo wa kusafirisha.

Jana Jumamosi vita vilikuwa vikali kote katika eneo la Gaza ambapo Wapalestina wengi wanaripotiwa kuuawa. Wizara ya afya ilitangaza kwamba idadi ya waliouawa jana asubuhi ni watu 83.

Israel ilianzisha mashambulizi katika mji wa Rafah Mei 7, 2024 hata baada ya miito dhidi ya hatua hiyo kutoka kwa viongozi mbali mbali na shirika la umoja wa mataifa.

Mashambulizi hayo juu ya eneo zima la Gaza yalianza kama njia ya kulipiza kisasi baada ya waasi wa kundi la Hamas kushambulia maeneo mbali mbali ya Israel Oktoba 7, 2023.

Watu wapatao 1200 waliuawa siku hiyo huku wengine zaidi ya 200 wakishikwa mateka na Hamas.

Website | + posts