Home Habari Kuu Watu zaidi ya 30 wauawa na mioto ya mwituni Algeria

Watu zaidi ya 30 wauawa na mioto ya mwituni Algeria

0
kra

Mioto ya mwituni inaongezeka nchini Algeria na kuua watu wasiopungua 34 na kujeruhi wengine 26.

Joto kali zaidi linashuhudiwa nchini humo.

kra

Mioto hiyo ilizuka kote nchini Algeria hasa katika maeneo ya pwani katika Bahari ya Mediterania kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema jana Jumatatu kuwa wanajeshi 10 ni miongoni mwa watu 34 waliofariki. Iliongeza kuwa watu wasiopungua 26 walijeruhiwa na wengine wapatao 1,500 kuhamishwa.

Wizara ya Ulinzi imesema wanajeshi waliofariki walinaswa kwenye mioto ya mwituni wakati wakihama kwani miale na moshi ilisambaa kwa kasi.

Joto kali zaidi linashuhudiwa kote katika mataifa yaliyo kando na Bahari ya Mediterania.

Katika nchi jirani Tunisia, halijoto za nyuzi 49 za Selisiasi zimerekodiwa na mioto ya mlimani imezuka magharibi mwa nchi hiyo.

Mioto ya mwituni pia imezuka kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Rhodes na kuwalazimisha watalii wengi kuhama.

Website | + posts