Watu wapatao 50 wameripotiwa kufariki kati ya Jumanne na Jumatano wiki hii mjini Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kutokana na mvua kubwa inayoshuhudiwa.
Mvua hiyo pia imesababisha uharibifu maeneo ya kusini mwa Kivu ikisababisha maporomoko ya ardhi,kuanguka kwa nyumba na mito kuvunja kingo.
Msemaji wa mji wa Bukavu Joseph Mugisho Zihalirwa, amesema watu 19 wameaga dunia na wengine 5 kujeruhiwa wialayani Kadutu, wakiwemo jamaa 11 wa familia moja waliosombwa kutoka na kuvufurika kwa mto.
Mjini Kananga,watu 22 wmeripotiwa kufariki na zaidi ya nyumba 15 kusombwa kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyoletwa na mvua.