Home Habari Kuu Watu wawili zaidi wafariki kutokana na mafuriko hapa nchini

Watu wawili zaidi wafariki kutokana na mafuriko hapa nchini

Mwaura amethibitisha kuwa visa 53 vipya vimeripotiwa kote nchini na visa vingine 54 vya kuhara vimezuka katika gereza la Nyeri.

0
Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura.

Watu wawili zaidi wameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na janga hilo hapa nchini kuwa 291.

Aidha watu 75 zaidi hawajulikani waliko na wengine 188 zaidi wamejeruhiwa kulingana na takwimu zilizotolewa na msemaji wa serikali Isaac Mwaura leo Alhamisi.

Mwaura aliyasema hayo Alhamisi katika shule ya Lily’s mtaani Githurai, kaunti ya Kiambu, wakati wa kutoa chakula cha msaada pamoja na nguo kwa waathiriwa wa mafuriko katika eneo hilo, zilizotolewa na serikali ya taifa.

Wakati huo huo Mwaura amethibitisha kuwa visa 53 vipya vimeripotiwa kote nchini na visa vingine 54 vya kuhara vimezuka katika gereza la Nyeri.

Alisema eneo la Kimende lililokumbwa na maporomoko ya udongo siku ya Jumanne, limetangazwa kuwa eneo hatari na limezingizrwa.

Kundi la asasi mbali mbali pamoja na maafisa wa msalaba mwekundu linatekeleza shughuli za uokoaji katika eneo hilo.

Website | + posts