Home Habari Kuu Watu wawili wafariki kutokana na mlipuko wa gesi Embakasi

Watu wawili wafariki kutokana na mlipuko wa gesi Embakasi

0

Watu wawili wameripotiwa kuaga dunia kufuatia mlipuko wa gesi ya kupikia uliotokea mtaani Embakasi kaunti ya Nairobi usiku wa manane Ijumaa.

Msimamizi wa Polisi wa Embakasi Wesley Kimeto amethibitisha kuwa wawili waliofariki walikuwa mtu mzima mmoja na mtoto .

Juhudi za maafisa kutoka shirika la msalaba mwekundu zilisaidia kuwaokoa watu 271 wanaopokea matibabu katika vituo tofauti vya afya.

Majeruhi 167 wanapokea matibabu katika hospitali ya Mama Lucy wakiwemo watu wazima 142 na watoto 25, wanaotibiwa kutokana na matatizo ya kuvuta gesi

Majeruhi wengine saba walipewa rufaa katika hospitali ya rufaa ya kikuu cha Kenyatta na 7 na wengine 17 katika hospitali Kenyatta.

Kwa mjibu wa walioshuhudia mkasa huo, moto ulienea katika majenengo yaliyokuwa karibu.

Website | + posts