Home Kaunti Watu wawili wafariki katika ajali ya barabarani Embu

Watu wawili wafariki katika ajali ya barabarani Embu

0

Watu wawili walifariki Jumamosi mchana baada ya matatu kupoteza mwelekeo na kuwagonga waliokuwa wakitembea kwa migu nje ya hospitali ya Embu level Five.

Aliyeshuhudia kisa hicho Ann Murugi, alisema alikuwa amebebwa na pikipiki kabla ya matatu hiyo kuwagonga kwa nyuma.

Alisema matatu hiyo iliwagonga watu wawili nje ya hospitali ya Embu level Five na mwingine mmoja karibu na afisi za huduma center mjini Embu.

Walioshuhudia walisema wahudumu kadhaa wa bodaboda pia waligongwa na matatu hiyo.

Wakazi wa eneo hilo wametoa wito kwa serikali kukagua magari yote kuhakikisha yanaafikia sheria za trafiki.

Website | + posts