Home Habari Kuu Watu wawili wafariki katika ajali ya barabarani Baringo

Watu wawili wafariki katika ajali ya barabarani Baringo

Kamishna wa kaunti ya Baringo Stephen Kutwa, alisema miongoni mwa waliofariki ni mwalimu na mwanafunzi.

0

Watu wawili wamefariki leo Jumamosi kufuatia ajali ya barabarani, iliyohusisha basi la shule ya wavulana ya Kapsabet katika eneo la Patkawanin katika barabara ya Karbaret-Marigat,kaunti ya Baringo.

Akithibitisha ajali hiyo, kamishna wa kaunti ya Baringo Stephen Kutwa, alisema miongoni mwa waliofariki ni mwalimu na mwanafunzi.

Wanafunzi wengine 24 walijeruhiwa, watano kati yao walipata majeraha mabaya na walipelekwa katika hospitali za Kimishenari za Kabarnet na Marigat, na ile ya matibabu maalum ya Baringo.

Basi hilo lilikuwa limewabeba wanafunzi 61 wa jografia wa kidato cha pili na mwalimu mmoja, waliokuwa kwa ziara ya masomo katika ziwa Bogoria, Baringo kusini.

Kulingana na usimamizi wa shule hiyo, basi hilo lipoteza mwelekeo na kubingiria mara kadha.

Website | + posts