Home Habari Kuu Watu watatu wafariki baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi Garissa

Watu watatu wafariki baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi Garissa

Gari hilo lilikuwa limewabeba wahudumu 10 wa afya ajali hiyo ilipotokea.

0

Takriban watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya gari walimokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi katika kaunti ya Garissa.

Waathiriwa hao walikuwa wakisafiri kati ya eneo la Egge Dam na Bogyar katika barabara ya  Dadaab-Garissa, ajali hiyo ilipotokea takriban umbali wa kilomita 10 na mji wa Dadaab.

Kaimu kamishna wa kaunti ya Garissa Solomon Chesut akithibitisha kisa hicho kwa njia ya simu, alisema watu wawili walifariki papo hapo huku mwingine akifariki akipokea matibabu katika kituo kimoja cha afya.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali moja ya eneo hilo kwa matibabu.

Kulingana na Chesut, gari hilo lilikuwa limewabeba wahudumu 10 wa afya ajali hiyo ilipotokea.

Hili ndilo tukio la kwanza la uvamizi kutumia vilipuzi tangu barabara ya Garissa -Dadaab ilipofunguliwa upya baada ya kuharibiwa n mvua ya El Nino.

Website | + posts