Home Kimataifa Watu wanne wakamatwa kuhusiana na jaribio la mapinduzi Burkina Faso

Watu wanne wakamatwa kuhusiana na jaribio la mapinduzi Burkina Faso

Mamia ya watu waliandamana katika mji mkuu Ouagadougou, kuunga mkono serikali ya kijeshi.

0
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traoré.

Siku moja baada ya serikali ya kijeshi ya Burkina Faso kutangaza kuwa imetibua jaribio la mapinduzi, utawala wa nchi hiyo umesema umewatia nguvuni maafisa wanne kuhusiana na jaribio hilo.

“Washukiwa hao huenda walihusika katika majaribio hayo dhidi ya usalama wa taifa,” alisema kiongozi wa mashtaka Ahmed Ferdinand Sountoura.

Aidha kulingana na kiongozi huyo wa mashtaka, maafisa wengine wawili walitoroka.

Jaribio hilo linajari mwaka mmoja tangu Kapteni Ibrahim Traoré kunyakua mamlaka, kupitia mapinduzi ya pili nchini humo ndani ya miezi minane.

Mwendesha huyo mashtaka wa kijeshi, alisema uchunguzi umeanza na ameomba mashahidi kujitokeza kufuatia kile alichokiita kuwa majaribio ya kuyumbisha nchi.

Mamia ya watu waliandamana katika mji mkuu Ouagadougou, kuunga mkono serikali ya kijeshi.

Aidha, serikali ilisimamisha shughuli za jarida la habari la lugha ya Kifaransa Jeune Afrique, ikilishutumu kwa kuchapisha makala yanayokashifu vikosi vya jeshi.