Watu wanne wanahofiwa kufariki baada ya jengo kuporomoka mtaani Pangani, kaunti ya Nairobi.
Watu wengine 15 waliijeruhiwa katika ajali hiyo na wanapokea matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Nairobi.
Kulingana na ripoti ya polisi, wengi wa majeruhi walikuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo hilo, ikidokeza kuwa uchunguzi umeanzishwa kubainisha chanzo cha tukio hilo.
Visa vya mijengo kuporomoka vimeshuhudiwa katika kaunti ya Kiambu katika siku za hivi maajuzi, huku kisa cha hivi punde cha nyumba kuporomoka kikiripotiwa katika eneo la Mirema.