Home Vipindi Watu wanne wa familia moja waangamia katika mkasa wa moto

Watu wanne wa familia moja waangamia katika mkasa wa moto

0

Watu wanne wa familia moja walifariki Jumatano usiku kufuatia mkasa wa moto katika Kijiji  cha Boiman Nyandarua Magharibi, katika kile kinachoaminika kuwa shambulizi la moto

Miongoni mwa wale walioangamia katika mkasa huo wa moto ni pamoja na ajuza mmoja wa umri wa miaka 85, mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 36 na wajukuu wake wawili walio na umri wa miaka kumi na Tano mtawalia.

John Mwangi, mwanawe mwendazake alisema walisikia kamsa kutoka nyumba yao, kabla ya kuelekea katika juhudi za kuokoa familia.

Nyumba hiyo iliyo na vyumba vitatu vya kulala, inasemekana ilikuwa imefungwa kwa upande wa nje na kufanya iwe vigumu kwa wanne hao kutoroka.

Wakazi wametoa wito kwa maafisa wa usalama kuchunguza kisa hicho.

Website | + posts