Home Kimataifa Watu waliozuru makazi ya Kiptum kabla ya kifo chake wakamatwa

Watu waliozuru makazi ya Kiptum kabla ya kifo chake wakamatwa

kra

Watu watatu kati ya wanne waliozuru makazi ya mwanariadha mshikilizi wa rekodi ya dunia Kelvin Kiptum siku nne kabla ya kifo chake wamekamatwa na wanachunguzwa.

Watatu hao ambao bado hawajatambuliwa, walipelekwa kwanza katika kituo cha polisi cha Kaptagat kaunti ya Elgeyo Marakwet kabla ya kuhamishiwa Iten.

kra

Wapelelezi wa kaunti ya Elgeyo Marakwet anakotoka Kiptum, wanachunguza watu hao kufahamu kuhusu ziara yao baada ya babake Kiptum kwa jina Samson Cheruiyot kutilia shaka ujio wao baada ya kifo cha mwanawe.

Washukiwa hao wanne waliitwa na afisa mkuu wa upelelezi wa jinai wa kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Mzee Cheruiyot alifahamisha maafisa hao wa polisi kuhusu ujio wa watu wanne ambao hakuwafahamu nyumbani kwake kijiji cha Chepsamo, wadi ya Kaptarakwa, eneo bunge la Keiyo Kusini na akataka wachunguzwe.

Kulingana naye, watu hao hawakujitambulisha vizuri siku hiyo.

Alitambua watatu hao katika kituo cha polisi cha Kaptagat pamoja na gari walilokuwa wakitumia likazuiliwa kituoni humo.

Website | + posts
Kimutai Murisha
+ posts