Home Habari Kuu Watu sita wafariki katika shambulizi la majangili Pokot Magharibi

Watu sita wafariki katika shambulizi la majangili Pokot Magharibi

0

Takribani watu sita Jumanne asubuhi,  kwenye shambulizi la majambazi katika sehemu ya Sarmach kaunti ya Pokot Magharibi.

Mauaji hayo yalitokea baada ya makabiliano kati ya wafugaji na wezi wa mifugo.

Watu wengine 16 walijeruhiwa na wanapokea matibanbu katika hospitali tofauti katika kaunti hiyo.

Kulingana na wakazi, watu watatu ambao walikuwa wakifuata mifugo walioibiwa walipigwa risasi wakati wa makabiliano baina ya wezi hao na maafisa wa usalama, ilhali majambazi watatu waliokuwa wameiba idadi ya mifugo isiyojulikana waliuawa na wananchi.

Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi wa Pokoti ya kati Nelson Omwenga, alisema waliojeruhiwa wakati wa makabiliano hayo wamelazwa katika hospitali mbalimbali wakiuguza majeraha.

Aidha wakazi wa eneo la Pokot, walisema kundi la maafisa wa usalama kutoka asasi mbalimbali, liliwarushia wananchi gurunedi waliokuwa wakitazama baada ya shambulizi hilo.

Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na naibu wa Gavana Robert Komolle na naibu Spika wa bunge la kaunti ya Pokot Magharibi Victor Sigwat, walishutumu hatua hiyo ya maafisa wa usalama.

“Kundi hilo la maafisa wa asasi mbali mbali za usalama limefanya jambo la kusikitisha ambalo halijawai onekana tangu uhuru, la kuwarushia gurunedi wananchi wasio na hatua,”  walisema viongozi hao.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Pokot Magharibi Peter Katam amesema uchunguzzi kuhusu tukio hilo umeanza.

Aidha alisema maofisa wa usalama wataimarisha doria katika sehemu hiyo.

Website | + posts