Home Habari Kuu Watu kadhaa wauawa kwenye mashambulizi ya Israel Rafah

Watu kadhaa wauawa kwenye mashambulizi ya Israel Rafah

0
kra

Watu kadhaa wamefariki kwenye mashambulizi ya makombora ya Israel kwenye kambi moja inayokaliwa na wapalestina katika eneo la Rafah kusini mwa eneo la Gaza. Kambi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kama eneo salama.

Kulingana na shirika la “Palestine Red Crescent Society” wengi wa waliofariki walichomeka kwenye hema zao katika eneo la Tal as-Sultan.

kra

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi hayo kulingana na Red Crescent ni 40, huku shirika la habari la Reuters likisema kwamba msemaji wa wizara ya Afya ya Gaza Ashraf al-Qudra aliweka idadi hiyo kuwa watu 35 na wengine wengi wakaachwa na majeraha.

Walioshuhudia mashambulizi hayo waliambia wanahabari kwamba makombora manane yalirushwa kwenye kambi hiyo Jumapili saa tatu kasoro robo usiku kulingana na saa za eneo hilo.

Israel ilisema kwamba roketi nane za wapiganaji wa Hamas zilirushwa kutoka eneo la Rafah mahali ambapo wanajeshi wake wameendelea kushambulia hata baada ya mahakama ya kimataifa ya haki ICJ kuagiza kwamba ikomeshe mashambulizi hayo.

Jeshi la Israel limesema pia kwamba lililenga majengo yanayotumiwa na Hamas huko Rafah na kwamba walitumia silaha sahihi baada ya kupokea taarifa sahihi za kijasusi.

Mkuu wa utumishi wa eneo la West bank wa kundi la Hamas na afisa mwingine mkuu wanaoaminika kuhusika na mashambuli dhidi ya Israel wanasemekana kufariki kwenye shambulizi hilo.

Baada ya shambulizi hilo majeruhi kadhaa wamekuwa wakimiminika kwenye hospitali ya muda ya kamati ya kimataifa ya shirika la Msalaba Mwekundu katika eneo la Rafah.

Website | + posts