Watu 84 walifariki kupitia ajali za barabarani katika wiki ya kwanza ya mwezi Januari mwaka 2024.
Kulingana na takwimu za mamlaka ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani, NTSA idadi ya mwaka huu ya vifo ni ya juu ikilinganishwa na vifo 72 vilivyonakiliwa ndani ya juma la kwanza mwaka 2023.
Kati ya idadi ya waliofariki mwaka huu, abiria wanaotembea kwa miguu ndio wengi wakiwa 31, wakifuatwa na waendeshaji wa pikipiki 23, huku madereva saba wa magari wakifariki.
Abiria sita waliobebwa kwa pikipiki walipoteza maisha yao katika kipindi hicho cha kati ya Januari 1 na 7 mwaka huu, na mwendeshaji baiskeli mmoja akaangamia.