Home Habari Kuu Watu 8 wafariki kwa ajali Nakuru

Watu 8 wafariki kwa ajali Nakuru

0

Watu wanane wamefariki kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha magari kadhaa mapema Jumannne katika kaunti ya Nakuru.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Ngata katika barabara kuu ya Eldoret-Nakuru -Nairobi, na ilihusisha gari dogo na malori mawili.

Yamkini lori hilo lilikata breki na kupoteza mwelekeo na kugonga gari dogo na lori jingine.

Waliofariki walikuwa wakisafiri kuelekea Kisii na wanajumuisha watu wazima sita na watoto wawili.

Watu wanane walifariki papo hapo huku wengine saba wakipokea matibabu hospitalini.

Website | + posts