Home Habari Kuu Watu 5 wafariki, wengine wajeruhiwa kwenye ajali Timboroa

Watu 5 wafariki, wengine wajeruhiwa kwenye ajali Timboroa

0

Watu watano walifariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi kufuatia ajali iliyotokea katika eneo la Mlango Tatu kwenye barabara ya Nakuru-Eldoret. 

Watu watatu walifariki katika eneo la ajali lakini wawili zaidi wakaaga dunia wakati wakitibiwa katika hospitali ndogo ya Eldama Ravine walikokimbizwa majeruhi wa ajali hiyo.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:40 usiku, kwa mujibu wa Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS.

Maafisa wa NPS kutoka kituo cha polisi cha Timboroa walifika eneo la ajali haraka kudhibiti hali.

Uchunguzi wa awali unaashiria kuwa ajali hiyo ilihusisha basi na magari mengine matatu likiwemo gari aina ya  Toyota Probox.

Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ndogo ya Eldama Ravine ikisubiri kufanyiwa upasuaji.