Mahakama moja ya kijeshi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imewahukumu kifo watu 37 kwa kujaribu kuipindua serikali mwezi Mei.
Miongoni mwa watu hao ni pamoja na raia sita wa kigeni, ambapo watatu kati yao ni raia wa Marekani, wengine wakitoka Ugelgiji,Canada na Uingereza.
“Mahakama hii inawahumuku kifo kwa kujihusisha na makosa ya jinai, hukumu ya kifo kwa kushambulia, hukumu ya kifo kwa ugaidi,” alisema Rais wa Mahakama hiyo Freddy Ehume, alipokuwa akitoa hukumu ya watu 51 katika kesi iliyoanza mwezi Juni,2024.
Mahakama hiyo ya kijeshi iliwahukumu kifo washtakiwa 37, kati ya 51.
Jaribio hilo la mapinduzi ya serikali linadaiwa kutekelezwa katika jiji Kuu Kinshasa Mei 19, 2024.
Washamuliaji hao kwanza walivamia makazi rasmi ya spika wa bunge la taifa hilo, kabla ya kuelekea katika makazi ya Rais.
Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, walisema kundli la watu 20 waliokuwa wamejihami, walitekeleza mashambulizi hayo.