Watu wawili wamefariki baada ya dereva wa basi walimokuwa wakisafiria kushindwa kulidhibiti na basi hilo.
Hali hiyo ilisababisha basi hilo kubingiria kwenye mtaro katika eneo la Gitaru katika kaunti ya Kiambu.
Watu wengine 50 walijeruhiwa huku 40 kati yao wakisemekana kuwa katika hali mahututi.