Kisa kinachoshukiwa kuwa cha kuvuja kwa gesi ya nitrate oxide nchini Afrika Kusini kimesababisha vifo vya watu 16, kwa mjibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Waathiriwa ni pamoja na wanawake na watoto ambao walivuta gesi hiyo katika mtaa mmoja wa mabanda wa Boksburg, ulio mashariki ya Johannesburg.
Uvujaji huo unadaiwa kusababishwa na uchimbaji dhahabu usio halali katika sehemu hiyo.
Gesi ya nitrate oxide hutumiwa na wachimba migodi wasio halali kutafuta dhahabu kutoka kwa mchanga ulioibwa kutoka migodi iliyoachwa.
Mkasa huo umetokea miezi sita pekee baada ya trela moja ya kusafirisha gesi kulipuka mkesha wa Krismasi na kusababisha vifo vya watu 41 mjini humo.