Home Habari Kuu Watu 15 waangamia kufuatia mvua kubwa

Watu 15 waangamia kufuatia mvua kubwa

0

Takriban watu 15 wamefariki kutokana na mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa inasema mvua hiyo itaendelea hadi mwezi Januari mwakani.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu, kufikia jana Jumapili, nyumba 15,264 zilikuwa zimeathiriwa na mifugo wapatao 1,067 kufariki kutokana na athari za mvua kubwa.

Ekari 241 za mashamba pia zimeharibiwa na mafuriko yanayotokana na mvua inayoendelea kunyesha nchini.

Watu sita waliripotiwa kuaga dunia kutokana na mvua akiwemo nyanya mwenye umri wa miaka 85 na watahiniwa wawili waliomaliza mtihani wa KCPE wiki jana.

Waathiriwa walisombwa na mafuriko eneo la Elwak kaunti ya Mandera siku ya Ijumaa.

Mtu mwingine mmoja alifariki baada ya nyumba yake kusombwa eneo la Kisauni, kaunti ya Mombasa Alhamisi usiku huku wengine wawili wakiangamia katika kaunti za Kwale na Meru.

Website | + posts