Home Habari Kuu Watu 1,214 wamefariki kwa ajali za barabarani tangu Januari 1 mwaka 2024

Watu 1,214 wamefariki kwa ajali za barabarani tangu Januari 1 mwaka 2024

Ogut ameongeza kuwa wasafiri wanaotembea kwa miguu wanaongoza kwa waliofariki wakifuatwa na waendeshaji pikipiki ,abiria wa magari na madereva wakifuata katika nafasi za tatu na nne mtawalia.

0

Mamlaka ya usafiri nchini NTSA imesema kuwa watu 1,214 wamefariki kupitia ajali za barabarani katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita .

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NTSA Christine Ogut, amesema takwimu hizo zinaogofya ikiwa ni ongezeko la asilimia 5 kutoka kwa idadi ya waliofariki katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka uliopita.

Ogut ameongeza kuwa wasafiri wanaotembea kwa miguu wanaongoza kwa waliofariki wakifuatwa na waendeshaji pikipiki ,abiria wa magari na madereva wakifuata katika nafasi za tatu na nne mtawalia.

Jumla ya watu 3,609 waliangamia kwenye ajali za barabarani mwaka uliopita huku 4,690 wakiangamia mwaka 2022.