Home Kimataifa Watu 119 waangamia kutokana na tetemeko la ardhi nchini Nepal

Watu 119 waangamia kutokana na tetemeko la ardhi nchini Nepal

0

Watu wapatao 119 wameripotiwa kufariki kwenye tetemeko kubwa la ardhi lililotekea nchini Nepal Ijumaaa usiku.

Tetemeko la ukubwa wa 5 nukta 6 katika vipimo vya ritcha magharibi mwa Nepal, na kubomoa nyumba za udongo zilizoporomoka na kuwalazimu wenyeji kukimbilia usalama wao.

Tetemeko hilo lilisikika hadi mjini New Delhi nchini India, takriban kilimoita 500 kutoka eneo la tetemeko.

Mitetemeko ya radhi ni maarufu sana nchini Nepal.