Home Taifa Watu 10 wafariki kwenye ajali Mai Mahiu

Watu 10 wafariki kwenye ajali Mai Mahiu

0

Watu kumi walifariki jana Jumamosi kwenye ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Mai Mahiu huku wengine wakiachwa na majeraha.

Ajali hiyo ya saa sita mchana ilihusisha trela na gari la kubeba abiria 14.

Walioshuhudia walisema kwamba trela ilipoteza mwelekeo kabla ya kugonga gari hilo la abiria ambayo lilikuwa limejaa abiria. OCPD wa Naivasha Stephen Kirui alithibitisha ajali hiyo akisema kwamba watu wengine walikimbizwa hospitalini wakiwa na majeraha.

Inaripotiwa kwamba waliokuwa kwenye gari hilo la kubeba abiria ni watu wa familia moja waliokuwa wakienda kuhudhuria hafla ya kifamilia ajali ilipotokea.

Tukio hilo lilisababisha msongamano mkubwa wa magari.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here