Home Habari Kuu Watoto wawili wafariki katika mkasa wa moto Kirinyaga

Watoto wawili wafariki katika mkasa wa moto Kirinyaga

0

Polisi katika kaunti ya kirinyaga wanachunguza kisa cha moto kilichosababisha vifo vya watoto wawili, katika kituo cha biashara cha kagumo kaunti ya Kirinyaga.

Mkasa huo ulitokea saa mbili usiku, ambapo watoto wawili wenye umri wa miezi minne waliteketea kwenye moto huo.

Kulingana na polisi, mama ya watoto hao wawili alikuwa ameenda sokoni kununua chakula cha jioni, wakati mkasa huo ulipotokea.

Wakaazi wa Kagumo na wazima moto kutoka serikali ya kaunti ya kirinyaga, walikumbwa na changamoto walipojaribu kuzima moto huo.

Mwakilishi wodi wa eneo hilo David Wangui, ambaye alifika katika eneo la mkasa huo alisema zaidi ya nyumba 20 za kupangisha ziliteketea .

Kamishna wa Kaunti ya Kirinyaga Hussein Alasow, alisema moto huo ulianza katika moja ya nyumba hizo, kabla ya kuenea na kufikia nyumba nyingine .

Miili ya watoto hao ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Kerugoya.