Home Kaunti Watoto 6 wafariki kwa moto Kericho

Watoto 6 wafariki kwa moto Kericho

0

Watoto wa familia moja wameteketea hadi kufariki mapema leo Jumatatu kufuatia mkasa wa moto ulioteketeza nyumba yao mtaani Kiptenden, eneo bunge la Kipkelion Magharibi, kaunti ya Kericho.

Watoto hao walikuwa wamelala wakati wa mkasa huo wa moto ambao chanzo chake hakijabainika.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo.

Juhudi za majirani kuwaokoa watoto hao ziliambulia pakavu kutokana na moto mkali ulioteketeza nyumba hiyo ya mbao.

Website | + posts