Home Habari Kuu Watoto 16 wanaoaminika kutekwa nyara waokolewa Kayole, Nairobi

Watoto 16 wanaoaminika kutekwa nyara waokolewa Kayole, Nairobi

0

Maafisa wa polisi waliokoa watoto 16 wanaoaminika kutekwa nyara kutoka kwa nyumba moja ya makazi katika mtaa wa Kayole kaunti ya Nairobi.

Watoto hao wa umri wa kati ya miaka miwili na 16 wanajumuisha wasichana 6 na waliokolewa kwenye paresheni ya Jumapili Februari 18, 2024 usiku.

Watu wawili mmoja raia wa Kenya na mwingine raia wa Tanzania waliokuwa wameweka watoto hao walikamatwa na maafisa wa polisi.

Inaaminika kwamba walikuwa wanapanga njama ya kusafirisha watoto hao ambao wanatoka sehemu mbali mbali za Kenya na Tanzania kinyume cha sheria.

Mkuu wa polisi katika kaunti ya Nairobi Adamson Bungei alielezea kwamba watoto waliookolewa walipelekwa kwenye makazi ya watoto yatima katika eneo la Kayole.

Bungei anahimiza umma kufahamisha polisi kuhusu visa vyovyote vya kushukiwa huku akielezea kwamba washukiwa waliokamatwa wanachunguzwa ili kufahamu walikokuwa wanapanga kupeleka watoto hao.

Website | + posts