Home Biashara Watengenezaji bidhaa wakongamana Nairobi

Watengenezaji bidhaa wakongamana Nairobi

0
kra

Mamia ya watengenezaji bidhaa, wataalam wa ufadhili wa biashara na wataalam wa sekta ya mpangilio wa huduma katika mitandao wako jijini Nairobi kwa maonesho ya kimataifa ya siku mbili ili kubadilishana mawazo kuhusu changamoto zinazokabili biashara, miundombinu ya ufadhili na masoko ya bidhaa katika kanda ya Afrika mashariki.

Mwandalizi wa maonesho hayo ambaye ni makamu wa rais wa kampuni ya uuzaji wa mipangilio ya huduma katika mitandao ya “Newgen”, Vivek Bhatnagar amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wanaohudhuria kupata maarifa kuhusu maendeleo ya hivi punde na mabadiliko ya haraka kuhusu ufadhili wa biashara duniani hasa kwa kuzingatia masoko ya bara Afrika.

kra

Kwa mujibu wa Bhatnagar, washiriki wanaweza kukutana na kupata ushauri wa wataalam kutoka kampuni ya “Newgen”, ili kujifunza mengi kuhusu biashara zao na usambazaji wa bidhaa kuwawezesha kutumia teknolojia ya kisasa kurahisisha shughuli zao.