Home Habari Kuu Watalii wawili wauawa nchini Uganda

Watalii wawili wauawa nchini Uganda

Polisi nchini Uganda wamesema wanawasaka wanaoshukiwa kuwa waasi wa Allied Democratic Forces, ADF baada ya kuwapiga risasi na kuwaua raia wawili wa kigeni na mmoja wa Uganda katika Bustani ya Queen Elizabeth wilaya ya Kasese, magharibi mwa nchi hiyo.

Msemaji wa polisi Fred Enanga alisema, “tumesajili shambulizi la kiuoga la kigaidi la watalii wawili wa kigeni na raia mmoja wa Uganda katika bustani ya Queen Elizabeth.’’

Gazeti la Daily Monitor limeandika kuwa, kulingana na taarifa ya polisi, waasi hao walichoma moto gari walilokuwa wakitumia hadi likawa jivu.

“Jeshi letu lilichukua hatua mara moja baada ya kupata taarifa hizo na wanawasaka wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi la ADF. Rambirambi zetu ni kwa familia za waathiriwa,’’ Enanga alisema.