Home Kaunti Watahiniwa wahamishiwa shule za maeneo salama Lamu

Watahiniwa wahamishiwa shule za maeneo salama Lamu

0
Mtihani wa KCPE na KPSEA wakamilika.

Watahiniwa wa mtihani wa darasa la nane KCPE na wa gredi ya sita KPSEA ambao wamekuwa wakisomea kwenye shule za maeneo ambayo huathiriwa na utovu wa usalama kila mara katika kaunti ya Lamu, wamehamishiwa shule za maeneo salama.

Mitihani hiyo imeanza leo Jumatatu kote nchini.

Kulingana na naibu kamishna wa eneo la Lamu Magharibi Gabriel Kioni, watahiniwa wa shule za maeneo kama vile Juhudi, Salama, Poromoko na Pandanguo watafanyia mitihani yao katika shule zilizo karibu ambazo zinachukuliwa kuwa katika maeneo salama.

Watahiniwa 2,440 katika vituo 70 katika kaunti ndogo ya Lamu Magharibi wanafanya mtihani wa KPSEA huku wengine 2,346 katika vituo 68wakifanya mtihani wa KCPE.

Mtahiniwa mmoja wa shule ya msingi ya Hongwe atafanya mtihani wake wa KCPE katika zahanati ya Mpeketoni baada ya kufanyiwa upasuaji wiki kadhaa zilizopita.

Huu ndio mtigani wa mwisho wa darasa la nane KCPE nchini, mtaala wa elimu unapobadilishwa kutoka mfumo wa 8.4.4 hadi mfumo mpya wa CBC.

Website | + posts