Home Habari Kuu Watahiniwa wa KCPE kujiunga na sekondari Januari 15

Watahiniwa wa KCPE kujiunga na sekondari Januari 15

0

Wanafunzi waliokalia mtihani wa darasa la nane mwaka huu, KCPE watajiunga na shule za upili Januari 15 mwaka ujao.

Haya yametangazwa na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, alipoongoza hafla ya uteuzi wa wanafunzi hao iliyofanyika mapema leo Jumatatu katika shule ya upili ya Lenana.

Machogu ameongeza kuwa wanafunzi watatumia mfumo wa NEMIS ambao unapatikana mtandaoni, kujisali kabla ya kujiunga na shule za sekondari walizoteuliwa.

Wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE wanaweza wakabaini shule walizoteuliwa na masharti yanayohitajika kwa kusakura tovuti ya Wizara ya Elimu ambayo ni www.education.go.ke. ama www.kemis.education.go.ke.

Website | + posts