Wafanyikazi wote wa umma watakaostaafu watapata ufueni ikiwa mswaada wa kamati ya fedha bungeni utapitishwa kuea sheria.
Mswaada huo unapendekeza kuishuritisha hazina kuu kuwalipa wastaafu wote ndani ya miezi mitatu baada ya kustaafu.
Kamati ya fedha bungeni imefanyia mabadiliko sheria za hazina ya kustaafu kipengee cha 189,kitakachoishurutisha serikali kuwalipa wastaafu wote katika kipindi fulani.
Endapo mswaada utafanywa sheria serikali italazimishwa kuwalipa wafanyikazi wanaostaafu katika kipindi fulani punde baada ya kuondoka kazini.