Home Habari Kuu Wasimamizi wa mitihani watakiwa kuzingatia miongozo iliyopo

Wasimamizi wa mitihani watakiwa kuzingatia miongozo iliyopo

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaokiuka miongozo ya kusimamia mitihani

0

Huku mitihami ya kitaifa inapokaribia, wasimamizi wa mitihami hiyo wametakiwa kutekeleza uadilifu na kuzingatia miongozo iliyopo.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaokiuka miongozo ya kusimamia mitihani.

Kwa mujibu wa Machogu, usalama utaimarushwa wakati wa kipindi cha mitihani katika maeneo yanayoshuhudia ukosefu wa usalama.

Taifa hili linapojiandaa kupokea mvua ya El Nino, Machogu alisema wizara yake imeweka mikakati ya kushugulikia dharura yoyote itakayoyokea.

Kuhusu mfumo wa kutoa alama kwa wanafunzi, Machogu alidokeza kwa mfumo utakaotumika katika mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, ni masomo mawili tu ambayo yatakuwa ya lazima kujumlishwa ikilinganishwa na idadi ya hapo awali ya masomo matano.

Masomo hayo ni Hisabati pamoja na somo lingine moja kati ya Kiswahili, Kingereza au somo la ishara.

Baraza la Kitaifa la Mitihani, KNEC kisha litakadiria masomo mengine matano yaliyofanywa vyema na mtahimiwa.

Machogu aliyasema hayo katika mkutano na wadau wengine jana Jumatatu, wakati wa kuzindua kipindi cha mitihani ya kitaifa nchini.

Mitihani ya KCPE, KPSEA na KCSE inatarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu.