Home Kimataifa Wasimamizi wa mashirika ya serikali watakiwa kuzingatia sheria

Wasimamizi wa mashirika ya serikali watakiwa kuzingatia sheria

0

Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabia Nchi na Misitu Aden Duale ametoa wito kwa wasimamizi wa mashirika ya serikali yaliyo chini ya wizara hiyo, wahakikishe mashirika yao yanatekeleza shughuli kuambatana na sheria na kanuni zilizoko.

Duale alizungumzia sheria ya usimamizi wa fedha za umma na ile ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa na huduma za umma na pia ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za umma, kuwa kanuni na sheria muhimu zinazofaa kuzingatiwa nyakati zote.

Aliyasema hayo wakati wa mkutano na wakuu wa mashirika ya kiserikali, iliyoandaliwa katika idara ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri Duale pia aliwahimiza watii sheria akisema kuwa sheria ndio itahakikisha ufanisi kama taasisi na kuwakinga dhidi ya sakata zozote.

“Zingatieni sheria wakati wote. Ni sheria itakayowahakikishia ufanisi kama taasisi, na kuwalinda dhidi ya matatizo,” alisema Duale.

Akiwatahadharisha maafisa dhidi ya kutoa ushauri wa kupotosha kwa afisi yake  Duale aliwahimiza maafisa hao wakuu wahakikishe kwamba mipango, miradi na hatua zinatekelezwa kwa wakati ufaao.

Website | + posts